KAULIMBIU: "TIME FOR CHANGES" | Karibu kwenye Portal Rasmi ya Serikali ya Wanafunzi KISO.

KILIMANJARO INSTITUTE STUDENT'S ORGANIZATION

Serikali ya Wanafunzi KITM (2025/2026)

Motto: Time for Changes

Kuhusu KISO

Serikali ya Wanafunzi KISO ni chombo rasmi cha uwakilishi wa wanafunzi kilichoanzishwa kwa mujibu wa katiba ya chuo kwa lengo la kusimamia haki, maslahi na maendeleo ya wanafunzi.

KISO hufanya kazi kwa karibu na uongozi wa chuo ili kuhakikisha mazingira bora ya masomo, ustawi na mshikamano wa wanafunzi. KISO ina wajibu wa kusikiliza sauti za wanafunzi na kushughulikia changamoto zao.

Maadili ya KISO
  • Uadilifu
  • Uwajibikaji
  • Uwazi
  • Ushirikishwaji
  • Nidhamu

Maono (Vision)

Kuwa serikali ya wanafunzi yenye uongozi bora, uwazi, uwajibikaji na mchango chanya katika maendeleo ya chuo na jamii kwa ujumla.

Dhamira (Mission)

Kuwakilisha wanafunzi kwa haki na ufanisi, kulinda maslahi yao, na kushirikiana na uongozi wa chuo katika kuboresha mazingira ya kujifunza.

Uongozi wa KISO

Joseph Yona Odende

Rais wa KISO (President)

"Kwa niaba ya Serikali ya Wanafunzi KISO, nawakaribisha wanafunzi wote kushirikiana nasi katika kujenga mazingira bora ya masomo na ustawi. Ushirikiano wenu ni msingi wa mafanikio yenu. KISO ipo kwa ajili yenu."

Huduma za Serikali ya Wanafunzi

KISO inatoa huduma mbalimbali kwa lengo la kuboresha ustawi wa wanafunzi, masomo na ushiriki wao katika maendeleo ya chuo.

Jinsi Tunavyotoa Huduma

1. Wasilisha changamoto/wazo
2. KISO inapokea na kuchambua
3. Majadiliano na uongozi
4. Mrejesho kwa mwanafunzi

Matukio na Matangazo

Eneo hili litatumiwa kwa ajili ya matukio, video, mikutano, ziara na matamasha yajayo.